Kuhusu Elimu Kiganjani

Watanzania wengi wanatafuta majibu ya matatizo ya kila siku mtandaoni (kukojoa kitandani, harufu ya mdomo, kujiamini, pesa), lakini majibu mengi yako kwa Kiingereza kigumu, au ni ya uongo yanayouza dawa feki.

Elimu Kiganjani inaleta suluhisho hizo karibu nawe: vijitabu vifupi, vyenye michoro, kwa Kiswahili rahisi ambacho hata mtoto wa darasa la tatu anaelewa, kwa bei ya kikombe cha chai.

Kila kijitabu kimeandikwa kutoka tafiti, miongozo ya madaktari na vyanzo vinavyoaminika, na vyanzo vimeorodheshwa ndani yake. Lengo letu si pesa tu, ni kuisaidia jamii.